KOCHA SIMBA TUNATAKA KUSHINDANA NA AL AHLY, TP MAZEMBE AFRIKA.

KOCHA SIMBA TUNATAKA KUSHINDANA NA AL AHLY' TP MAZEMBE AFRIKA





KOCHA  wa klabu ya Simba, Didier Gomes Da Rosa amefunguka kwamba malengo yake ni kuhakikisha anatengeneza kikosi imara ambacho kitakuwa na uwezo wa kushindana dhidi ya timu kubwa barani Afrika kama TP Mazembe na Al Ahly, sambamba kuonesha upinzani kwa kila mashindano watakayoshiriki ndani na nje ya tanzania na afrika kwa ujumla.

Gomez alikuwa  rasmi kocha mkuu wa klabu ya Simba Jumapili ya Januari 24 akichukua nafasi ya Mbelgiji, Sven Vandenbroeck ambaye mapema mwaka huu , alijiuzulu nafasi hiyo ya ukocha,    muda mfupi tu baada ya kuifikisha Simba kwenye hatua ya Robo fainali ya michuano ya Ligi ya mabingwa Afrika, kwa kuitoa timu ya FC PLATNUM kwa jumla ya mabao 4-1,kwenye uwanja wa mkapa dar es salaam.

Gomez akiwa kama kocha mkuu wa timu hio, tayari amekwishasimamia mazoezi ya kikosi chake kwa siku tatu mfululizo akikiandaa kikosi chake kwa  ajiri  ya michuano ya Simba Super Cup iliyoanza jana huku ikishirikisha timu tatu ambazo ni Al Hilal, TP Mazembe na mwenyeji Simba.

Akiwa katika mazoezi ya timu yake ,kocha huyo alionekana kukazia zaidi katika ufundishaji wa pasi fupifupi na mazoezi magumu.

Aidha, akizungumzia mipango yake, Gomez alisema: “Nafurahi kuwepo hapa, nimejifunza vitu vingi ndani ya muda mfupi, vijana wangu wanaonekana kuwa na Molali kubwa na wanajituma sana mazoezini, kiufupi tuu niseme nafurahi kuwa katika klabu  yangu hii mpya ya Simba SC, pia nafurahishwa saana na wachezaji wa timu yangu wanavyojituma"

Kocha huyo aliongezea kwa kusema “Malengo yetu ni kufanya vizuri kwenye kila michuano tunayoshiriki, lakini tunaendelea kuwekeza nguvu kubwa katika kuhakikisha tunakuwa na kikosi imara ambacho kitaweza kushindana dhidi ya timu kubwa kama TP Mazembe na Al Ahly kwenye michuano ya Afrika"

“Simba ni miongoni mwa klabu 20 bora barani Afrika na inaheshimika sana mbele ya wapinzani wake, hususani wakiwanyumbani kwenye uwanja wa Mkapa, hivyo nasi ni lazima tuhakikishe tunakuwa  washindani wa kweli dhidi ya wapinzani wetu,”

Mapema jana gomez alianza ukurasa wake wa maisha kunako klabu ya Simba kwa ushindi mnono wa mabao 4-1 dhidi ya mabingwa wa Sudan AL HILAL, huku  Wachezaji wake wakionesha jitihada kubwa sana,  wakipambana kupata matokeo,

Comments

Post a Comment