MSHINDI SIMBA SUPER CUP KUBEBA SHILINGI 15 MILION
Uongozi wa klabu ya Simba umeweka wazi kwamba zawadi zitakazotolewa kwa bingwa wa michuano ya Simba Super Cup ni kiasi cha shilingi milioni 15 pamoja na kikombe na medali, michuano hio ilianza kutimua vumbi tangu Januari 27, 2021.
Ofisa Habari wa wa timu hiyo, Haji Manara amesema kuwa tumepanga kutoa zawadi hiyo pamoja na kutoa burudani kwa mashabiki ambao watajitokeza kutazama mashindano hayo yanayofanyika kwa mara ya kwanza ndani ya ardhi ya Tanzania.
Katika mashindano hayo ni timu tatu tuu, ndio ambazo zinashiriki ikiwa ni pamoja na wenyeji Simba,TP Mazembe ya Congo na Al Hilal ya Sudan.
Klabu ya Simba ilianza mchezo wake wa ufunguzi kwa ushindi wa mabao 4-1 dhidi ya Al Hilal, huku mchezo wa pili ulikuwa ni jana, kati ya Al Hilal dhidi ya TP Mazembe, huku Al Hilal akiibuka na ushindi wa mabao 2-1.
Kilele cha mashindano hayo ni kesho Januari 31 ambapo Simba itacheza na TP Mazembe na mshindi atapatikana hio kesho, Uwanja wa Mkapa.
Manara amezungumzia pia kuwa, baada ya mchezo huo wa mwisho kutakuwa na tafrija (after party) ambayo itafanyika jijini Dar es Salaam, maeneo ya ‘Kidimbwi Beach’
Aidha, Manara amesema pia kuelekea kilele cha mashindano hayo hio kesho, kutakuwa na msanii wa Bongo Fleva kutoka kundi la WCB Mwanadada Zuchu ambaye Anatarajiwa kutoa burudani katika mchezo huo wa mwisho wa michuano hiyo utakaopigwa kesho Jumapili, Januari 31, 2021 kati ya Simba vs TP Mazembe.
Manara amesema:-"Tumejipanga na tunawaomba mashabiki wajitokeze kwa wingi kushangilia na kuona burudani, pia atakuwepo Mwanadada Zuchu kwa ajiri ya kutupatia burudani kidogo"
Mashindano hayo yanafikia tamati siku ya kesho juma pili, ikiwakutanisha Mabingwa wa Tanzania Simba dhidi ya mabingwa toka congo TP Mazembe, mchezo utakao pigwa katika uwanja wa Mkapa kuanzia mida ya saa 10 alasiri, Bingwa wa michuano hio atajinyakulia pesa za kitanzania taslimu shilingi milion 15, pamoja na kikombe na medali.
Comments
Post a Comment