BARBARA; TULITAKA KUWAALIKA YANGA KWENYE SIMBA SUPER CUP

CEO SIMBA TULITAKA KUWAALIKA YANGA SUPER CUP;


Ofisa Mtendaji Mkuu wa Simba, Barbara Gonzalez amesema walikuwa na wazo la kuishirikisha klabu ya Yanga katika mashindano yao ya ‘Simba Super Cup’.Mashindano hayo ya Simba Super Cup yanashirikisha timu tatu pekee yaliyoanza jana kwa wenyeji kuwaalika al hilal, kabla ya wageni hao kucheza na TP Mazembe na kisha wenyeji SIMBA kumalizana na TP MAZEMBE kwenye Uwanja wa Benjamin Mkapa, Dar es Salaam.


Barbara alisema "walikuwa na wazo la kuwashirikisha mahasimu wao, Yanga katika michezo hiyo, lakini baada ya majadiliano na viongozi wezake ya kama watakubali au la, wakaamua kuahirisha, uamuzi huo"


CEO huyo wa Simba alisema ,wazo hilo lilikuwa kwa nia njema, kwani kwao hawakuwa wakihitaji kuonyeshana ubabe kwa upinzani walionao, bali kutumia kama njia mojawapo ya kujiandaa kwa ajiri ya mashindano ya kimataifa. “Ni kweli, tulikuwa na wazo la kuiandikia barua kabisa klabu ya Yanga kushiriki kwenye mashindano ya Simba Super Cup, lakini tulifikiria mimi pamoja na viongozi wezangu wa klabu ya simba mara mbili kama wanaweza kutujibu na kushiriki kwa wakati huu, ama wataelewa vinginevyo"


“Baada ya majadiliano ya muda tukaona tuliahirishe wazo hilo hadi wakati mwingine. Tunataka kufanya mashindano haya kufanyika kila mwaka na inawezekana kabisa wakati mwingine tukawaandikia wenzetu wa Yanga kushiriki,” alisema Barbara.


Simba inashiriki mashindano ya Ligi ya Mabingwa Afrika, ikiwa katika hatua ya makundi, imeanza mazoezi juzi kwa ajili ya kujiandaa na mzunguko wa pili lakini pia mashindano hayo ya kimataifa yanayotarajiwa kuanza mwezi february, ikiwa kundi moja na timu za AL AHLY, AS VITA pamoja na AL MEREKH.


Mashindano ya Simba Super Cup yanashirikisha timu za Simba (Tanzania) ambae ni mwenyeji, TP Mazembe (DR Congo) na A Hilal ya Sudan.


Katika mchezo wa kwanza, Simba imecheza na Al Hilal na kumalizika kwa simba kuibuka na ushindi wa 4-1, shukrani kwa mabao ya Raly Bwalya, Chikwende na mabao mawili ya kiungo mshambuliaji Bernard Morrison, SIMBA inatarajiwa kushuka tena dimbani januari 31, kumalizana na TP Mazembe.

Comments