MORRISON ATAJA SIKU ANAYOIKUMBUKA NDANI YA SIMBA;
KIUNGO mshambuliaji wa klabu ya Simba, Bernard Morrison amesema kwamba miongoni mwa vitu ambavyo anavikumbuka zaid ndani ya klabu yake ya Simba ni pamoja na siku yake ya utambulisho iliyofanyika kwenye tamasha la Simba day.
Mghana huyo aliibukia kunako klabu ya Simba akitokea Klabu ya Yanga ambapo dili lake limekuwa na utata hasa katika masuala ya kimkataba.
klabu ya yanga ambayo ni Mabosi wake wa zamani wa mchezaji huyo, wanadai kwamba mchezaji huyo ni mali yao kwa kuwa alisaini dili la miaka miwili huku Morrison akiweka wazi kwamba alisaini na klabu hiyo dili la miezi sita tuu.
Sakata lake lilitinga kunako Shirikisho la Soka Tanzania, (TFF) ambapo lilisikilizwa kwa muda wa siku tatu kisha ikaamuliwa kuwa mchezaji huyo ni huru kwa kuonekana makosa ya kimkataba, kati ya Yanga na Morrisoni huku ikiwa pamoja na suala la saini na mhuri.
Aidha,Morrison amesema:"Ninaikumbuka sana siku ile ya utambulisho kwa mashabiki, Uwanja wa Mkapa, namna ambavyo walinipokea na kunishangilia kama mchezaji wao, ilikuwa furaha kwangu na ipo kwenye kumbukumbu zangu, " .
Kwa sasa mchezaji huyo,ndani ya Simba amekuwa hana nafasi katika kikosi cha kwanza cha timu hiyo, huku sababu kubwa ikielezwa kuwa ana matatizo ya afya jambo ambalo limemuweka nje ya uwanja kwa muda mrefu,tangu mwishoni mwa mwaka jana.
Comments
Post a Comment