KONDE BOY AWASILI DAR, KUIWAHI SIMBA SUPER CUP

 KONDE BOY AREJEA KUIWAHI AL HILAL SIMBA SUPER CUP;


Kiungo nyota mshambuliaji wa klabu ya Simba,raia wa msumbiji  Luis Miquissone 'Konde Boy' amewasili rasmi leo jijini Dar es Salaam, kuiwahi michuano ya simba super cup, akitokea kwao nchini Msumbiji, alipokuwa kwa ajili ya mapumziko mafupi na anatarajiwa kujiunga na kambi ya Simba iliyopo chini ya mkufunzi DIDIER GOMES DA ROSA, ikiwa  inajiandaa na mashindano hayo ya Simba Super Cup.

Miquissone amekuwa na mchango mkubwa katika ushindi wa Simba,tangu ametua kunako klabuni hapo,akitokea Msumbiji, huku akihusika katika mabao manane ya simba ndani ya ligi kuu tanzania bara,  akiwa amefunga bao moja na assisti saba, nyota huyo wa Simba alikuwa mapumzikoni huko kwao Msumbiji, baada ya kuisaidia team yake kutinga hatua ya makundi ya Ligi ya mabingwa Afrika  ikiiondosha FC Platimun kwa ushindi wa jumla ya mabao 4-1.

Miquissone aliyehusika kwenye mabao nane ya Simba akifunga bao moja na kuasisti mara saba kwenye michuano ya Ligi Kuu Bara, alikosekana katika michuano ya kombe la Mapinduzi iliyomalizika kwa Yanga kuibuka na ubingwa baada ya kuifunga Simba kwa mikwaju ya Penalti 4-3.

Michuano hio ya Simba Super Cup itashirikisha timu tatu za SimbaAl hilal na TP Mazembe huku ikitarajiwa kuanza kutimua vumbi siku ya al hamis kwenye uwanja wa mkapa ambapo Simba wataianza karata yake kwa kucheza dhidi ya Al Hilal ya Sudan.

Mapema leo timu ya Al hilal imetua katika uwanja wa mwl julius nyerere,kwa ajiri ya michuano hio, huku wakitarajiwa kuanza karata yao dhidi ya simba sc, siku ya al hamis majira ya saa 11 jion kwenye uwanja wa mkapa Dar es salaam.


Comments