NYOTA YANGA WAWEKWA CHINI YA MADAKTARI

NYOTA WAWILI YANGA WAWEKWA CHINI YA UANGALIZI WA MADAKTARI;



Taarifa rasmi kutoka kunako kwa Uongozi wa klabu ya Yanga umesema kuwa nyota wao wawili Yacouba Sogne na Saido Ntibazonkiza bado wapo kwenye uangalizi wa jopo la madaktari,ili kuhakikisha usalama wa afya zao ikiwa fit kwa asilimia 100 kabla ya kurejea uwanjani, mapema mwez february kwa ajiri ya mzunguko wa pili wa ligi kuu tanzania bara maarufu kama VPL.

Kikosi hicho  kilichopo chini ya mkufunzi Kocha Mkuu, Cedric Kaze kimeshawasili kambini na kilianza mazoezi rasmi jumatatu Januari 25,Kigamboni.

Aidha, Meneja wa Yanga, Hafidh Saleh amesema kuwa maendeleo ya wachezaji wao wawili  Saido Ntibazonkiza na Yacouba Songne ni mazuri,huku wakitarajiwa kuwa fit zaid mpaka pale ligi itakaporudi.

"Wachezaji  wote ambao wameshawasili kambini wanaendelea vizuri na tayari mazoezi yanaendelea ambapo ni Saido na Yacouba hawa bado hawajawa kwenye ubora wao kwa asilimia 100.

Aidha Hafidh amesema "Wachezaji hao bado wapo kwenye uangalizi wa jopo la madaktari na tunaamini kwamba watakuwa imara na watarejea uwanjani,ligi itakaporudi baada ya michuano ya chan".

Katika msimamo wa ligi,Yanga ipo nafasi ya kwanza ikiwa na pointi 44 baada ya kucheza jumla ya mechi 18,huku ikiwa haijapoteza mechi yoyote katika ligi kuu mpaka sasa.

Yacouba alipata majeraha kwenye mchezo wa hatua ya nusu fainali dhidi ya Azam FC,Ilikuwa ni kwenye Kombe la Mapinduzi uliochezwa Uwanja wa Amaan, visiwani Zanzibar, huku Ntibazonkiza alipata majeraha kwenye mchezo wa Ligi Kuu Bara dhidi ya Tanzania Prisons uliochezwa Uwanja wa Nelson Mandela, huku mchezo huo ukimalizika kwa sare ya 1-1

Licha ya kuwa majeruhi na kutokuwa fit kwa asilimia 100, Ntibazonkiza aliweza kuisaidia timu yake kubeba ubingwa wa mapinduzi cup baada ya kupiga penalt ya ushindi mbele ya watani zao Simba SC.

Yacouba na Ntibazonkiza ni maigizo mapya kunako klabu ya yanga,wakisainishwa kwa jitihada za mdhamini GSM chini ya engineer Hersi Said, na wamekuwa nyota wenye mchango mkubwa saana kwenye kikosi hicho cha kocha Cedrik Kaze.

Comments