RAIS MAGUFULI ATAHADHARISHA CHANJO YA COVID 19,ILIYOANZA KUTUMIKA MATAIFA MBALIMBALI

 RAIS MAGUFULI' TANZANIA HAITAKIMBILIA CHANJO YA COVID 19;


Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania John Pombe Magufuli ametahadharisha matumizi ya chanjo ya Covid 19 ambayo imeanza kutolewa katika mataifa mbalimbali duniani.

Aidha,Rais Magufuli akizungumza katika uzinduzi wa shamba la miti huko wilayani Chato mkoani Geita, amezungumzia pia kuhusu hali ya corona nchini Tanzania na kuwasihi wananchi kuendelea kuomba pamoja na kujifukiza, sambamba na kuchukua tahadhari.

‘’Tutaendelea kuchukua tahadhari, pamoja na kujifukiza, kusali na kuswali, huku tukiendelea na shughuli zetu, nawaasa wananchi  tule vizuri tushibe corona ashindwe kuingia kwenye miili yetu’’.

Aidha kuhusu uwepo wa aina mpya ya corona Rais Magufuli amesema kuwa kuna baadhi ya Watanzania wameenda kupata chanjo lakini bado hawajaleta aina mpya ya corona.

Aidha Rais Magufuli ameongezea kwa kusema kwamba ‘’Ninajua Kuna baadhi ya Watanzania, wameondoka ndani ya nchi na kukimbilia maeneo mengine na kwenda kwa ajir ya kupata chanjo hii ya covid 19, hvyo tuchukueni tahadhari tusije kusambaza na  huku nchini''

Rais Magufuli amesisitiza juu ya madhara ya chanjo, hususani kuwa hakuna chanjo za magonjwa sugu ya muda mrefu kama UKIMWI na SARATANI.

‘’tusiwe tunakimbilia masuala ya chanjo chanjo, si kila chanjo ina faida kwetu, ni lazima Watanzania tuwe macho, tuwe waangalifu, tutafanyiwa majaribio, tuendelee kumuomba Mungu wetu na tuendelee kuchukua tahadhari''.

Mapema mwezi huu,Serikali ya Uingereza imepiga marufuku abiria kutoka Tanzania na Jamuhuri ya Kidemokrasia ya Congo (DRC) kuzuia maambukizi ya aina mpya ya virusi vya corona.

"Ili kusaidia kuzuia kuenea kwa aina ya COVID-19 iliyogundulika Afrika Kusini, tunapiga marufuku abiria wote wanaoingia kutoka Tanzania na DRC kuanzia saa 10 alfajiri kesho (Ijumaa)," ameandika Bw Grant Shapps, waziri wa uchukuzi nchini Uingereza kupitia mtandao wake wa Twitter Alhamisi usiku.

Awali,naibu afisa mkuu wa matibabu Uingereza amesema''Watu waliopata chanjo bado wanaweza kuambukiza wengine virusi vya corona na hivyo basi, wameombwa kuendelea kutekeleza hatua za kuzuia kusambaa kwa ugonjwa huo''.

Comments